Kampuni ya mtandao wa Kijamii ya
Facebook imesema kuwa itanunua mtandao wa mawasiliano ya ujumbe mfupi
wa WhatsApp kwa kima cha dola bilioni kumi na sita, na nyongeza zaidi ya
dola bilioni tatu zitakazolipwa waanzilishi wa mtandao huo pamoja na
wafanyikazi wake.
Hiyo ndiyo biashara kubwa zaidi ya ununuzi kuwahi kutekelezwa na Facebook hadi kufikia sasa.
WhatsApp ni maarufu sana miongoni mwa vijana wanaotafuta kuepuka kulipia huduma ya kutuma ujumbe mfupi wa simu yaani SMS.
WhatsAp imeweza kuwasajili zaidi ya watumiaji milioni mia nne hamsini.
Katika taarifa, mwanzilishi wa Facebook Mark
Zuckerberg amesema kuwa mtandao huo upo njiani kuwaunganisha watu
bilioni moja jambo litafanya Facebook kuwa na thamani kubwa.
No comments:
Post a Comment