Pages

Ads 468x60px

LIKE THIS PAGE FIRST.

Tuesday, December 17, 2013

Tunisia:IMECHOSHWA NA SERIKALI YAO.


Wengi wanasema serikali inajikokota kupiga hatua tangu mapinduzi ya kiraia

Maelfu ya watu nchini Tunisia wamekuwa wakifanya maandamano mjini Sidi Bouzid, kitovu cha harakati za mapinduzi ya kiraia yaliyomwondoa mamlakani aliyekuwa Rais Zine el-Abidine Ben Ali miaka mitatu iliyopita.

Waandamanaji wanalalamikia ukosefu wa serikali kupiga hatua za kuridhisha tangu mapinduzi ya kiraia kufanyika.

Mji wa Sidi Bouzid ndiko kijana mmoja mchuuzi Mohamed Bouazizi alijiteketeza miaka mitatu iliyopita kuonyesha ghadhabu kwa ambavyo serikali ilikuwa inawanyanyasa raia wake.

Maandamano yaliyofuata tukio la kijana huyo kujiua, yalimwondoa mamlakani aliyekuwa Rais Zine el-Abidine Ben Ali na kuchochea maandamano mengine kama hayo katika nchi za kiarabu.

No comments:

Post a Comment