Pages

Ads 468x60px

LIKE THIS PAGE FIRST.

Sunday, December 15, 2013

MWENYEKITI WA CCM MKOA WA MWANZA, CLEMENT MABINA AUAWA KWA KUPIGWA NA WANANCHI

Aliyekuwa mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza MABINA ameuwawa na wananchi wenye hasira kali kwa kupigwa mawe huko maeneo ya Kiseke jijini mwanza.

Chanzo cha kuuwawa ni kwamba mabina aliwanyang'anya ardhi wananchi hao na kesi ikawa mahakamani na leo mchana mabina bila kibali cha mahakama alikuwa anapanda miti na kujenga msingi wa nyumba ndipo wanachi wakaenda kumhoji iweje anapanda miti na kuweka msingi kwenye viwanja hivyo ilhali kesi ipo mahakamani.?

Mabina akaanza kutoa lugha chafu na kurusha risasi hewani Risasi zilipomuishia na kufanikiwa kumuua raia m1 kwa risasi ndipo wananchi wenye hasira kali wakamrudia kumpiga wakiwa na mapanga, mawe na kila dhana ya kijadi, jambo lililopelekea umauti kumkuta. Mauaji yametokea mchana wa leo majira ya saa 7 

No comments:

Post a Comment