Pages

Ads 468x60px

LIKE THIS PAGE FIRST.

Sunday, December 15, 2013

DONDOO ZA BONDENI ZA MADIBA NELSON MANDELA, ENDELEA KUFATILIA.


1461669_10201924456245794_688868881_n_9e4de.jpg


Leo ndio siku ya mazishi ya Mwana wa Mama Afrika, Nelson Rolihlahla Mandela. Anazikwa kijijini kwao Qunu.

Mandela anayetoka kwenye kabila la Xhosa alizaliwa Julai 18, 1918 kijijini Mvezo, kando ya mto Mbashe, Wilaya ya Umtata, Makao Makuu ya Jimbo la Transkei.


Ukoo wa Mandela una mahusiano na Ukoo wa Kifalme wa Thembu. Baba yake Mandela, Gadla Henry Mphakanyiswa alikuwa Chifu kwa damu na kwa desturi. Naye akathibitishwa kuwa Chifu wa Mvezo na Mfalme wa himaya ya Thembu.


Mandela mwenyewe alizaliwa na jina Rolihlahla, ikiwa na maana ' Mwenye kuvuta matawi ya miti'. Na kwa lugha yao ina maana ya ' Msumbufu'.

Na hakika, Mandela amekuwa ' Msumbufu' kwa utawala wa kibaguzi hadi pale waliposalimu amri.


Mandela anasimulia, kuwa kumekuwa na hekaya sizizo za kweli kwenye kabila lao, kuwa naye ( Mandela) alikuwa mmojawapo katika mlolongo wa kurithishwa Uchifu kwenye himaya ya Thembu.

 Kwamba ingefika wakati naye Mandela angetawazwa kuwa Chifu. Mandela analikanusha hilo, anasema;(P.T)


" Although I was a member of the royal household, I was not among the privileged few who were trained for rule. Instead, as a descendant of the Ixhiba house, I was groomed, like my father before me, to counsel the rulers of the tribe."( Long Walk to Freedom, pg.5)

Kwamba ingawa alizaliwa katika ukoo wa Kichifu, lakini, hakuwa mmoja waliokuwa na fursa ya kupata mafunzo ya kuwa watawala.

 Lakini, kwa vile ana chimbuko la koo la Ixhiba, aliandaliwa, kama baba yake, kuwa mshauri wa watawala wa kabila lao.


Mandela anasimulia, kuwa katika miaka ya baadae ya utotoni, alibaini, kuwa baba yake hakuwa tu mshauri wa watawala, bali, aliwatengeneza watawala ( Kingmaker).


Naam, Mandela anazikwa kijijni kwao Qunu. Tumeona, kuwa hiki si kijiji alichozaliwa Mandela, alizaliwa Mvezo. Lakini, huko baba yake Mandela alilazimika kuhama na kwenda Qunu. Ni baada ya kutoelewana na mtawala.


Katika mazishi ya leo, wengi wamealikwa na Serikali ya Afrika Kusini kwenda kumsindikiza Mandela kwenye safari yake ya mwisho.


Lakini, kuna mtu mmoja ambaye inasemekana hayumo kwenye orodha ya waalikwa, ni Askofu Desmond Tutu. Huyu ni rafiki wa miaka mingi wa Nelson Mandela, na si marafiki tu, wawili hawa, kabla ya Mandela kukamatwa, waliishi nyumba jirani kwenye kitongoji cha soweto. Ndio, walikuwa majirani wa kuombana chumvi.


Je, ni kwanini jirani wa Mandela wa miaka mingi, Askofu Desmond Tutu, hayumo kwenye orodha ya watakaokwenda kumzika Mandela?
HABARI ZOTE ZIKO HAPA BOFYA HAPA  >>HABARI ZETU

No comments:

Post a Comment