Pages

Ads 468x60px

LIKE THIS PAGE FIRST.

Monday, October 21, 2013

DAWA YA MADREVA WALEVI SASA IMEPATIKANA.

 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma DR. Rehema Nchimbi, Kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma Suzan Kaganda na kaimu Mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini Ester Mgongolwa wakienda kupokea maandamano yaliyofanyika siku ya usalama Barabarani.
 Askali wa Jeshi la wananchi wa Tanzania [JWTZ] wakiongoza maandamano ya siku ya usalama Barabarani yaliyofanyika juzi mkoani Dodoma


 Waendesha Bodaboda mjini Dodoma wakiandamana katika maandamano ya amani yaliyoanzia kitio cha polisi kati kuelekea viwanja vya barafu wakati wa maadhimisho ya usalama barabarani

 Pc Jerome Mbano akimuelekeza Mkuu wa mkoa wa Dodoma DR. Rehema Nchimbi jinsi kipima ulevi kwa madereva kinavyofanya kazi.
 Kipima Ulevi kitakachotumika na polisi wa usalama Barabarani kuwagundua madereva wanaoendesha vyombo vya usafili huku wakiwa wamelewa.

Na John Banda, Dodoma
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi amewataka madereva wa magari ya Abiria na mizigo  wanaopitia mkoa huo kuacha kutumia kilevi chochote ikiwemo viroba wanapokuwa Barabarani la sivyo kufutiwa Leseni zao.
Mkuu huyo wa mkoa alitoa kauri hiyo siku ya usalama Barabarani iliyofanyika kimkoa katika viwanja vya Barafu mjini Dodoma juzi.
Nchimbi alisema ulevi kwa madereva hao umekuwa ukiwasababishia kuwa wazembe barabarani pindi wanapokuwa wakiendesha magali ya abiria kwa maana ya mabasi na maroli ya mizigo na huwa ni chanzo cha ajali za mara kwa mara.
Dr huyo wa Farsafa alisema ana taarifa za kutosha za ulevi kwa baadhi ya madereva hao na hivyo atatumia jeshi la polisi kuwanasa na kuwafutia leseni zao.
Aliongeza kuwa mbinu watakayotumia jeshi la polisi ni kuwapima madereva wote wanaoingia na kutoka ndani ya mkoa wa Dodoma  kwa kipimo maalumu cha kung’amua ulevi na atakaegundulika kuendesha akiwa amekunywa pombe au aina yoyote ya kilevi ikiwemo viroba atafutiwa leseni.
‘’Hivi sasa mkoa wetu unapoelekea kuwa jiji tunatakiwa pia kuwa mfano wa kuigwa na mikoa mingine kuhusu udhibiti wa madereva walevi, hivyo Dereva yoyote ili awe salama ahakikishe hajihusishi na ulevi ili aweze kupita mkoa huu akiwa salama la sivyo apitie juu ama kama kuna njia ya kuzunguka apite huko’’, alisema Dr. Chimbi
Aidha alisema zoezi hilo la kupima madereva walevi litaanzia kwa wale wa Daladala na Bodaboda ambao wamekuwa wakinyonya viroba hata wanapokuwa wanaendesha abiria wao bila kujali, aliwaagiza polisi kufavamia maeneo yote wanakopakilia na kuhakikisha wanawapima hapo hapo na atakaebainika uzi ni uleule wa kufutiwa leseni.
Awali akikielezea kipimia ulevi hicho kinachotumiwa na polisi wa usalama barabarani Pc Jerome Mbano alisema kipimo hicho kina uwezo wa kubaini kiwango cha pombe alichokunywa mtu hata kama alikunywa masaa 24 yaliyopita [jana yake]

No comments:

Post a Comment