Pages

Ads 468x60px

LIKE THIS PAGE FIRST.

Thursday, September 19, 2013

TAZAMA PICHA 4 ZA TUKIO LA JAMBAZI LILILOUWAWA NA POLISI KWA KUPIGWA RISASI JIJINI DAR.!


Mtu aliedhaniwa ni jambazi baada ya kuuwawa na Polisi eneo la Sukita Jijini Dar Es Salaam.
Kikosi cha Defender kinachopambana na majambazi, Kikosi cha polisi Magomeni
Wazee wa kazi mara tu baada ya kumaliza shughuli ya kupambani na majambazi na kufanikiwa kumuuwa mmoja.
Mmoja kati ya watu wanaodaiwa kupora fedha Vingunguti baada ya kuuwawa na polisi.
 
Jeshi la polisi kikosi cha kupambana na majambazi kimefanikiwa kumuua mmoja kati ya watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi mara baada ya kurushiana risasi na polisi eneo la SUKITA jijini Dar es Salaam.
Tukio hilo limetokea siku chache zilizopita maeneo ya SUKITA na taarifa kutoka eneo la tukio zinasema,watu hao wanadaiwa kupora kiasi kikubwa cha pesa katika duka moja la jumla na reja reja eneo la vingunguti jijini Dar es Salaam.

Taarifa zinasema majambazi hayo yalikuwa manne na yalikuwa na usafiri wa pikipiki na mara baada ya kupora wananchi walianza kuyazingira ndipo mmoja wapo aliyeshika mfuko wa fedha walizopora akaanza kuzirusha kwa wananchi na walivyoanza kuzigombea pesa hizo ndipo yakapata mwanya wa kutoroka eneo la tukio.

Hata hivyo taarifa ziliwafikia polisi ambao walikuwa doria na walipewa taarifa kuwa yanaelekea njia ya sukita na walipowawekea mtego wakanasa,na ndipo katika harakati za kuwakamata walianza kuwarushia risasi polisi,ndipo moja kati yao, alipigwa risasi ya kichwa na kufa papo hapo na mengine matatu yakatokomea kusikojulikana.

No comments:

Post a Comment