Pages

Ads 468x60px

LIKE THIS PAGE FIRST.

Tuesday, December 18, 2012

MALKIA AHUDHURIA MKUTANO WA MAWAZIRI

 Katika sherehe za mwisho za kuadhimisha miaka hamsini , tangu kuchukua uongozi malkia Elizabeth wa Uingereza ameweka historia ya kuwa mtawala wa kwanza katika kipindi cha zaidi ya karne mbili kuhudhuria mkutano wa baraza la mawaziri.
Malkia Elizabeth
Malkia akiwa katika mkutano wa baraza la mawaziri
Katika sherehe za mwisho za kuadhimisha miaka hamsini , tangu kuchukua uongozi malkia Elizabeth wa Uingereza ameweka historia ya kuwa mtawala wa kwanza katika kipindi cha zaidi ya karne mbili kuhudhuria mkutano wa baraza la mawaziri.
Vilevile, himaya ya uingereza katika eneo la Antarctic imepewa jina lake.
Akiwa katika mkutano wa mawaziri, aliketi kwenye kiti ambacho kwa kawaida hutumiwa na waziri mkuu David Cameron, ambaye alimwambia anaamini kuwa mara ya mwisho kwa mtawala wa kifalme kuhudhuria mkutano wa mawaziri ilikuwa ni katika kipindi ambacho Marekani ilikuwa ikipigania uhuru wake kutoka kwa waingereza.
Malikia aliondoka na zawadi ya zulia la kifahari lililonunuliwa na fedha zilizochangwa na mawaziri.
Baadae aliitembelea ofisi ya mambo ya nje ambapo waziri wa mambo ya nje William Hague alimwambia sehemu ya kusini ya himaya yake katika eneo la Antarctica limepewa jina la malikia Elizabeth kama heshima kwake.

No comments:

Post a Comment